Loading...

Salamu za Karibu.

Salamu za Karibu.

Dr. Salma Kitara

Mganga Mfawidhi

Hospitali ya Arusha Jiji ilianzishwa na kufunguliwa mnamo Tarehe 17 Oktoba, 2021 na Mheshimiwa Raisi Samia S. Hassan ikiwa ni Agizo la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa na lengo la kuimarisha utoaji wa Huduma za Afya ndani ya Halmashauri ya Arusha Jiji

Hospitali ya Arusha Jiji ilianzishwa ukiwa ni mkakati wa kuhakikisha Huduma za Mama na Mtoto, huduma za kudhibiti Magonjwa ya Kuambukizwa na yasiyo ya Kuambukizwa inatolewa katika ufanisi wa hali ya juu kutoka kwa Wataalamu wetu wabobezi. Pia, Hospitali ya Arusha Jiji inajumuisha idadi zaidi ya 4 kwa wodi za Binafsi kwa wagonjwa wanaopatiwa Huduma, wodi zaidi ya 10 za Umma pia kw wagonjwa wanaofika Hospitali kwa ajili ya kupatiwa Huduma za matibabu ya Afya kulingana na huduma wanayopaswa kupatiwa zikiwemo pia Huduma za malipo ya Papo Hapo, malipo kupitia Mifuko ya Bima za NHIF na CHF vilevile wale wagonjwa wanaoptiwa Huduma kwa Msamaha wa Malipo

Hospitali ya Arusha Jiji inajumuisha Vitengo / Huduma mbalimbali kulingana na changamoto za kiafya anazokutana nazo Mgonjwa katika jamii. Huduma hizo zikijumuisha zifuatazo;

  • Kitengo Wagonjwa wa Nje (OPD)
  • Kitengo Wagonjwa wa Ndani (IPD)
  • Kitengo cha Maabara
  • Kitengo cha dawa
  • Kitengo cha Mionzi
  • Kitengo cha Theatre ( Upasuaji )
  • Kitengo cha Lishe
  • Kitengo cha Uzazi wa Mpango (RCH)
  • Kitengo cha Mazoezi

Hospitali ya Arusha Jiji inajumuisha Rasilimali na Vitendea kazi vinavyotumiwa Wataalamu wetu wabobezi katika kutoa Huduma kwa wagonjwa. Miongoni mwa Rasilimali ninkama ifuatavyo;

  • 50+ Watumishi, Inajumuisha Wataalamu wa Afya wabobezi katika kutoa Huduma za Afya kwa watu katika jamii katika masuala mbalimbali ya huduma za Afya
  • 70+ Vifaa Inajumuisha Vitendea Kazi mbalimbali vinavyotumiwa na Watoa Huduma wetu wenye ufanisi mkubwa wa kazi kwa wagonjwa wanaofika kwa ajili ya matibabu
  • 150+ Samani Inajumuisha Samani zinazotumiwa na watoa huduma wetu wenye ufanisi wa hali ya juu katika kutoa huduma kwa wagonjwa wanaofika Hospitali
  • Huduma Masaa 24/7 Hospitali ya Arusha Jiji inatoa Huduma Masaa 24 kwa wagonjwa wanaofika kwa ajili ya kupata Huduma kutoka kwa Wataalamu wetu wabobezi katika Masuala ya huduma za Afya
  • Huduma Bora kwa Wateja Inajumuisha Huduma za Ushauri zikiwemo pia huduma nyingine za kwa wagonjwa wanaofika katika Hospitali ya Arusha Jiji
  • Hali ya Usalama ya Hali ya juu, Inajumuisha Huduma za usalama wa hali ya juu kwa wagonjwa ndani na nje ya Maeneo ya halmashauri ya Arusha Jiji

Hospitali ya Arusha jiji inatoa Huduma za Afya kwa kuzingatia Muongozo kutoka Wizara ya Afya Tanzania. Timu yetu ya wataalamu wa Afya ipo tayari kukusikiliza.

" Karibu sana Hospitali ya Arusha Jiji !! "

Tafadhali Andika Maoni Yako

Tafadhali Andika Maoni Yako Hapa kwa Ajira ya Kuboresha Huduma. Karibu sana!!