Hospitali ya Arusha Jiji inajumuisha Huduma mbalimbali za Matibabu zinazotolewa kwa wagonjwa wanaofika hospitali. Huduma hizi hutolewa na Wataalamu wetu wabobezi wa Masuala ya Afya. Huduma hizi ni kama zifuatazo;
1. HUDUMA YA KLINIKI YA MENO
Hospitali ya Arusha Jiji ina wataalamu Wabobezi katika Huduma ya Kliniki ya Meno kwa wagonjwa mbalimbali katika jamii. Baadhi ya Huduma ya matibabu ya Meno ni kama zifuatazo;
Miongoni mwa Takwimu za Huduma ya Kliniki ya Meno inayotolewa katika Hospitali ya Jiji la Arusha kutoka kwa wataalamu wetu wabobezi inajumuisha zifuatazo;
Kitengo / Mwaka
|
2021 (Wagonjwa)
|
2022 (Wagonjwa)
|
2023 (Wagonjwa)
|
2024 (Wagonjwa)
|
Chini Miaka 5 | 14 | 27 | 115 | 156 |
Chini Miaka 14 | 30 | 42 | 95 | 61 |
Zaidi Miaka 15 | 74 | 62 | 83 | 119 |
Hospitali ya Jiji la Arusha inatoa Huduma za Kliniki ya Meno kutoka kwa wataalamu wetu wabobezi. Huduma bora kwa kuzingatia utaalamu wa kutosha ili kuleta matokeo bora kwa wapokea huduma kutoka kwetu
2. HUDUMA YA UZAZI
Hospitali ya Arusha Jiji ina wataalamu Wabobezi katika Huduma ya Uzazi Macho kwa wagonjwa mbalimbali katika jamii. Baadhi ya Huduma za Uzazi zinazopatikana katika Hospitali ya Arusha jiji ni pamoja na zifuatazo;
Miongoni mwa Takwimu za Huduma za Uzazi zinazotolewa katika Hospitali ya Jiji la Arusha kutoka kwa wataalamu wetu wabobezi zinajumuisha kama ifuatavyo;
Kitengo / Mwaka
|
2021 (Wagonjwa)
|
2022 (Wagonjwa)
|
2023 (Wagonjwa)
|
2024 (Wagonjwa)
|
Wajawazito | 1483 | 3831 | 3881 | 964 |
Wagonjwa wa Nje (OPD) | 9887 | 20828 | 29016 | 7859 |
Wazazi | 174 | 1148 | 1653 | 410 |
Huduma ya Uzazi inatolewa katika Hospitali ya Jiji la Arusha kwa wapokea Huduma wote mara Kabla na Baada ya kujifungua kwa ubora wa hali ya juu kutoka kwa wataalmau wetu wabobezi ili kuhakikisha huduma bora zinatolewa kulingana na viwango vinavyohitajika na Wizara ya Afya Tanzania.
Tafadhali Andika Maoni Yako Hapa kwa Ajira ya Kuboresha Huduma. Karibu sana!!