Loading...

Huduma za Macho & Mionzi Tiba Ultra Sound

Huduma za Macho & Mionzi Tiba Ultra Sound

Hospitali ya Arusha Jiji inajumuisha Huduma za Matibabu mbalimbali kwa wagonjwa wanaofika. Huduma zinatolewa katika ufanisi wa hali ya juu kutoka kwa Wataalamu wetu wabobezi kama ifuatavyo;

1. HUDUMA YA MIONZI ULTRA SOUND

Hospitali ya Arusha Jiji ina wataalamu Wabobezi katika Tiba ya Mionzi kwa wagonjwa mbalimbali katika jamii. Miongoni mwa Huduma za Tiba Mionzi zinazotolewa katika Hospitali ya Arusha jiji ni pamoja na zifuatazo;

  • Screening ya Sehemu za Mwili
  • Screening ya Sehemu za Maungo ya Mwili (Joints)
  • Ushauri

Miongoni mwa Takwimu za Huduma ya Ultra Sound inayotolewa katika Hospitali ya Jiji la Arusha kutoka kwa wataalamu wetu wabobezi inajumuisha zifuatazo;

Kitengo / Mwaka
2021 (Wagonjwa)
2022 (Wagonjwa)
2023 (Wagonjwa)
2024 (Wagonjwa)
Wajawazito 1483 3831 3881 964
Wagonjwa wa Nje (OPD) 9887 20828 29016 7859
Wazazi 174 1148 1653 410

Hospitali ya Jiji la Arusha inatoa Huduma za Ultra Sound kutoka kwa wataalamu wetu wabobezi. Huduma bora kwa kuzingatia utaalamu wa kutosha ili kuleta matokeo bora kwa wapokea huduma kutoka kwetu


2. HUDUMA YA KLINIKI YA MACHO

Hospitali ya Arusha Jiji ina wataalamu Wabobezi katika Tiba ya Huduma za Macho kwa wagonjwa mbalimbali katika jamii. Miongoni mwa Huduma zinazotolewa kitengo cha Macho ni pamoja na zifuatazo;

  • Kutoa Ushauri wa Afya ya Macho
  • Kupima Macho (Afya ya Macho)
  • Kupima Uwezo wa Kuona
  • Kutibu Magonjwa mbalimbali ya Macho
  • Kupima Presha ya Macho

Miongoni mwa Takwimu za Huduma ya Kliniki ya Macho inayotolewa katika Hospitali ya Jiji la Arusha kutoka kwa wataalamu wetu wabobezi inajumuisha zifuatazo;

Kitengo / Mwaka
2021 (Wagonjwa)
2022 (Wagonjwa)
2023 (Wagonjwa)
2024 (Wagonjwa)
Chini Miaka 5 39 52 178 962
Chini Miaka 15 53 49 83 156
Zaidi Miaka 15 127 201 345 410

Hospitali ya Jiji la Arusha inatoa Huduma za Kliniki ya Macho kutoka kwa wataalamu wetu wabobezi. Huduma bora kwa kuzingatia utaalamu wa kutosha ili kuleta matokeo bora kwa wapokea huduma kutoka kwetu


Tafadhali Andika Maoni Yako

Tafadhali Andika Maoni Yako Hapa kwa Ajira ya Kuboresha Huduma. Karibu sana!!