Taarifa
Kambi Maalum ya Madaktari Bingwa wa Raisi Dkt. Samia Suluhu Hassani , ndani ya Hospitali ya Jiji Arusha. Tarehe: 20-24/05/2024
Hii ni Kambi Maalum ya Madaktari Bingwa wa Mheshimiwa Raisi Dkt. Samia Suluhu Hassan ndani ya Hospitali ya Jiji Arusha iliyoandaliwa kwa lengo la kuimarisha uwezo wa Wataalamu wa Afya ndani ya Tanzania. Kambi ilienda vizuri ikiambatana na ushirikiano wa hali ya juu kutoka kwa washiriki walioweza kufika.
Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani, ndani ya Hospitali ya Jiji Arusha. Tarehe: 17/05/2024
Haya ni Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Hospitali ya Jiji Arusha yakijumuisha Wauguzi mbalimbali wanaopatikana ndani ya Jiji la Arusha. Maadhimisho yalienda vizuri yakiambatana na Maandamano ya kuvutia.
Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano TANZANIA ndani ya Hospitali ya Jiji Arusha. Tarehe: 26/04/2024
Maadhimisho ya Sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (TANZANIA) yakijumuisha Wakazi, watumishi mbalimbali pamoja na viongozi mbalimbali yakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Felician Mtahengera kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha katika kushiriki shughuli mbalimbali zikiwemo Zoezi la Utoaji Damu, Upandaji wa Miti, ushauri wa masuala ya Afya pamoja na Ufanyaji usafi mazingira kuzunguka Hospitali ya Jiji la Arusha.
Ujio wa Timu Kazi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( TAKUKURU ) ndani ya Hospitali ya Jiji Arusha. Tarehe : 04/02/2024
Lilikuwa ni tukio la kuvutia ambapo Timu Kazi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( TAKUKURU )walifika katika Hospitali ya Jiji Arusha kuunga mkono jitihada za Hospitali yetu katika zoezi zima la utoaji wa huduma za Afya katika jamii. Zoezi lilienda vizuri likiandamana na upandaji wa Miti ya kuvutia ndani ya Hospitali ya Jiji Arusha
Kikao cha Asubuhi ( Morning Report) cha Wafanyakazi wa Hospitali ya Arusha Jiji
Hiki ni kikao cha Wafanyakazi wa Hospitali ya Arusha Jiji kinachofanyika Mara Nne ( Kwa siku Nne) kila Wiki kuzungumzia changamoto Mbalimbali za Kiutendaji wanazokutana nazo wafanyakazi. Pia, kikao hiki hutumiwa na wafanyakazi katika kushirikishana mawazo ya kujenga katika zoezi la utoaji huduma kwa wagonjwa.
Kliniki ya Mama na Mtoto, Hospitali ya Arusha Jiji. Tarehe: 23/02/2024
Hii ni huduma ya Kliniki ya Mama na Mtoto inayotolewa na kitengo cha Uzazi wa Mpango ( RCH ) Muda ni Kila Siku, kuanzia saa 02:00 Asubuhi hadi Saa 09:30 Mchana ikiwa na lengo la kufuatilia na kuhakikisha Maendeleo ya Mama na Mtoto katika jamii yanazingatia vigezo vinavyotakiwa na Wizara ya Afya. Pia huduma hii inahakikisha Maendeleo ya mtoto baada ya kuzaliwa yanakuwa vizuri ikijumuisha pia huduma za Ushauri wa uzazi wa Mpango kutoka kwa wataalamu wa Afya kutoka Hospitali ya Arusha Jiji
Zoezi la Uelimishaji jamii kuhusu Lishe, Radio TBC Arusha. Tarehe: 24/01/2024
Hili ni zoezi lililoandaliwa na radio TBC Arusha kwa kushirikiana na Wataalmau wa Afya ya Lishe kutoka Hospitali ya Arusha Jiji. Zoezi lilikuwa na lengo la kutoa elimu kwa jamii kuhusu kanuni bora za Lishe katika kujikinga na magonjwa mbalimbali. Zoezi lilifanyika vizuri na jamii ilifanikiwa kupata elimu kuhusu Afya ya Lishe kupitia Radio TBC Arusha
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Arusha Jiji, Dkt. Salma Kitara akikagua Ujenzi unaoendelea wa Jengo la Wagonjwa wa Nje, Hospitali ya Arusha Jiji. Tarehe: 19/02/2024
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Arusha Jiji, Dkt. Salma Kitara akikagua Ujenzi unaoendelea wa jengo linalotazamiwa kutumika kwa ajili ya Wagonjwa wa Nje katika Hospitali ya Arusha Jiji. Kwa ripoti inayoonesha kuwa Ujenzi unaendelea vizuri katika kuboresha Miundombinu ya Utoaji huduma kwa Wagonjwa
Mkuu wa Mkoa wa Arusha. Mhe. John Mongella akikagua Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Nje, Hospitali ya Arusha Jiji. Tarehe: 18/10/2023
Mkuu wa Mkoa wa Arusha akikagua ujenzi wa jengo la wagonjwa wa Nje unaonedelea katika Hospitali ya Arusha Jiji. Ujenzi unaendelea vizuri ikiwa ni Matazamio ya Hospitali hiyo kuimarisha miundombinu rafiki ya ufanyaji kazi kwa huduma za wagonjwa wa nje kutoka kwa wataalamu wabobezi wa Afya katika hospitali hiyo
Kliniki ya Mama na Mtoto. Muda : Kila siku, Saa 02:00 Asubuhi - Saa 09:30 Alasiri
Hii ni huduma ya Kliniki ya Mama na Mtoto inayotolewa na kitengo cha Uzazi wa Mpango ( RCH ) Muda ni Kila Siku, kuanzia saa 02:00 Asubuhi hadi Saa 09:30 Mchana ikiwa na lengo la kufuatilia na kuhakikisha Maendeleo ya Mama na Mtoto katika jamii yanazingatia vigezo vinavyotakiwa na Wizara ya Afya. Pia huduma hii inahakikisha Maendeleo ya mtoto baada ya kuzaliwa yanakuwa vizuri ikijumuisha pia huduma za Ushauri wa uzazi wa Mpango kutoka kwa wataalamu wa Afya kutoka Hospitali ya Arusha Jiji
Kampeni ya Kitaifa ya Chanjo ya SURUA / RUBELLA kwa Watoto. Tarehe : 15 - 18 /02/2024
Hii ni kampeni ya Kitaifa ya Chanjo ya SURUA / Rubella kwa watoto wa umri kuanzia Umri wa Miezi Tisa hadi Umri wa Miaka Mitano ikiwa na lengo la kuhakikisha Mtoto anapata kinga ya magonjwa ya Surua na RUBELLA ambayo yanaathiri afya ya Mtoto katika makuzi. Huduma hii ilitolewa na wataalamu wetu wabobezi katika Hospitali ya Arusha Jiji kwa ufanisi wa hali ya juu ikipata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wazazi wa watoto waliowaleta katika Hospitali ya Arusha jiji
Uanzishwaji wa Mfuko wa Mama na Mtoto Hospitali ya Arusha Jiji
Huu ni mkakati na utekelezaji wa malengo ya Wizara ya Afya katika kuhakikisha Afya ya Mama na Mtoto baada ya kujifungua inazingatiwa na kupatiwa uangalizi mzuri. Zikiwemo pia huduma za kukidhi mahitaji muhimu ya Mama mjamzito baada ya kujifungua ili kuimarisha Afya ya mtoto.
Kikao cha Mpango wa Mwaka Hospitali ya Arusha Jiji
Hiki ni kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Vikao wa Hospitali ya Arusha Jiji ikiwa ni sehemu ya kuimarisha mipango ya utekelezaji wa shughuli za utoaji Huduma za Afya kwa jamii