Loading...

Matukio

Matukio

Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano TANZANIA ndani ya Hospitali ya Jiji Arusha. Tarehe: 26/04/2024

Maadhimisho ya Sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (TANZANIA) yakijumuisha Wakazi, watumishi mbalimbali pamoja na viongozi mbalimbali yakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Felician Mtahengera kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha katika kushiriki shughuli mbalimbali zikiwemo Zoezi la Utoaji Damu, Upandaji wa Miti, ushauri wa masuala ya Afya pamoja na Ufanyaji usafi mazingira kuzunguka Hospitali ya Jiji la Arusha.

Ujio wa Timu Kazi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( TAKUKURU ) ndani ya Hospitali ya Jiji Arusha. Tarehe : 04/02/2024

Lilikuwa ni tukio la kuvutia ambapo Timu Kazi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( TAKUKURU )walifika katika Hospitali ya Jiji Arusha kuunga mkono jitihada za Hospitali yetu katika zoezi zima la utoaji wa huduma za Afya katika jamii. Zoezi lilienda vizuri likiandamana na upandaji wa Miti ya kuvutia ndani ya Hospitali ya Jiji Arusha

Kikao cha Asubuhi ( Morning Report) cha Wafanyakazi wa Hospitali ya Arusha Jiji. Tarehe: 26/02/2024

Hiki ni kikao cha Wafanyakazi wa Hospitali ya Arusha Jiji kinachofanyika Mara Nne ( Kwa siku Nne) kila Wiki kuzungumzia changamoto Mbalimbali za Kiutendaji wanazokutana nazo wafanyakazi. Pia, kikao hiki hutumiwa na wafanyakazi katika kushirikishana mawazo ya kujenga katika zoezi la utoaji huduma kwa wagonjwa.

Mganga Mfawidhi akikagua Ujenzi unaondelea wa Jengo la Wagonjwa wa Nje (OPD Complex). Tarehe: 19/02/2024

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Arusha Jiji, Dkt. Salma Kitara akikagua Ujenzi unaoendelea wa jengo linalotazamiwa kutumika kwa ajili ya Wagonjwa wa Nje katika Hospitali ya Arusha Jiji. Kwa ripoti inayoonesha kuwa Ujenzi unaendelea vizuri katika kuboresha Miundombinu ya Utoaji huduma kwa Wagonjwa. Hali ya ujenzi inaendelea vizuri, ikiwa ni Maboresho katika Miundombinu ya utoaji Huduma za Afya kwa wagonjwa wanaofika kupata huduma.

Mkuu wa Mkuu wa Arusha. Mhe. John Mongella akikagua Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Nje, Hospitali ya Arusha Jiji. Tarehe: 18/10/2023

Mkuu wa Mkoa wa Arusha akikagua ujenzi wa jengo la wagonjwa wa Nje unaonedelea katika Hospitali ya Arusha Jiji. Ujenzi unaendelea vizuri ikiwa ni Matazamio ya Hospitali hiyo kuimarisha miundombinu rafiki ya ufanyaji kazi kwa huduma za wagonjwa wa nje kutoka kwa wataalamu wabobezi wa Afya katika hospitali hiyo. Ujenzi unaendelea vizuri kwa ufanisi wa Wahandisi mahiri wa Ujenzi ikizingatiwa kufikia malengo na ubora wa Hospitali ya Arusha Jiji katika kuimarisha mazingira bora ya utoaji wa huduma kwa Wagonjwa wanaofika kupata huduma za Afya.

Uchangiaji wa Damu katika maeneo ya Halmashauri ya Arusha jiji. Tarehe: 2701/2024

Hili ni tukio lililoratibiwa na Wataalamu wetu wabobezi katika kutoa elimu juu ya umuhimu wa Uchangiaji Dawa. Timu yetu walifanya kazi nzuri ya kutoa huduma elimu ya umuhimu wa uchangiaji dawa pamoja na kuongeza uelewa wa huduma nyingine za Matibabu ya Afya juu ya namna za kujikinga na magonjwa mbalimbali zikiwemo elimu za lishe kwa wagonjwa

Elimu ya Lishe kutoka kwa Wataalamu Hospitali ya Arusha Jiji. Tarehe: 24/01/2024

Utoaji wa Elimu ya Lishe kutoka kwa Wataalamu wa Lishe ni zoezi lililofanyika katika Hospitali ya Arusha jiji ikiwa na lengo la kuwaelimisha wananchi katika jamii kuhusu ni kanuni zipi za Afya zinatakiwa zizingatiwe katika masuala ya lishe. Zoezi lilienda vizuri kutoka kwa wataalamu wetu.

Semina Elimu ya Huduma za Afya katika Ofisi za Tume ya Atomiki Tanzania ( TAEC), Njiro, Arusha. Tarehe: 17/12/2023

Hii ni Semina iliyofanyika katika ofisi za Tume ya Atomiki Tanzania (TAEC), Njiro Arusha iliyokuwa na malengo ya kutoa Huduma ya ushauri kwa watu katika jamii kutoka kwa Wataalamu wabobezi kutoka Hospitali. Semina ilifanyika vizuri kwa wapokea huduma iliyoongeza idadi ya wagonjwa katika hospitali ya Arusha Jiji

Semina ya Huduma ya Ushauri katika ofisi za VETA. Njiro, Arusha. Tarehe : 14/11/2023

Semina ilifanyika kwa ufanisi wa hali ya juu katika ofisi za VETA Njiro, Arusha ikiwa na lengo la kutoa huduma za Ushauri pamoja na huduma nyingine zikiwemo huduma za Lishe, huduma za Damu salama kutoka kwa wataalamu wetu wabobezi kutoka hospitali ya Arusha Jiji.

Zoezi la Uelimishaji jamii kuhusu Lishe, Radio TBC Arusha Tarehe: 07/12/2023

Hili ni zoezi lililoandaliwa na radio TBC Arusha kwa kushirikiana na Wataalmau wa Afya ya Lishe kutoka Hospitali ya Arusha Jiji. Zoezi lilikuwa na lengo la kutoa elimu kwa jamii kuhusu kanuni bora za Lishe katika kujikinga na magonjwa mbalimbali. Zoezi lilifanyika vizuri na jamii ilifanikiwa kupata elimu kuhusu Afya ya Lishe kupitia Radio TBC Arusha

Ujio wa Katibu Mkuu Taifa wa TUGHE ndani ya Hospitali ya Arusha Jiji, Tarehe : 20/10/2023

Huu ulikuwa ni wakati mzuri kwa Watumishi wa Hospitali ya Arusha Jiji kuwa na mazungumzo yenye tija na Katibu wa TUGHE Taifa ambapo Mgeni rasmi alihimizia Umoja na Mshikamano kwa wafanyakazi katika kuimarisha utoaji wa Huduma bora kwa wagonjwa wanaofika ndani ya Hospitali ya Arusha Jiji kupata huduma mbalimbali. Pia Mgeni rasmi alihimiza uwazi kwa watumishi katika kutimiza majukumu yao ya kila siku ili kuimarisha ufanisi wa ufanyaji kazi katika Hospitali ya Arusha jiji

Kikao cha Mafunzo cha SME Kwa Watumishi wa Hospitali ya Arusha Jiji. Tarehe : 04/09/2023

Hiki ni Kikao cha Mafunzo ambacho hufanyika katika Ukumbi wa Vikao wa Hospitali ya Arusha Jiji kikiwa na lengo la kufundishana, kubadilishana mawazo na kuchambua njia sahihi za kutumia katika kutatua changamoto mbalimbali za Kiafya wanazokutana nazo watu katika jamii. Pia, kikao hiki kinaongeza ufanisi wa ufanyaji kazi kwa watumishi ndani ya Hospitali ya Arusha Jiji katika utoaji huduma bora kwa wagonjwa. Kanzi Nzuri Timu !!.

Kikao cha Mganga Mfawidhi Dr. SALMA KITARA na Wafanyakazi Wote. Tarehe : 30/09/2023

Hiki ni Kikao hufanyika katika Ukumbi wa Vikao katika Hospitali ya Arusha Jiji ambapo Mwenyekiti wa Kikao hiko alikuwa Mganga Mfawidhi kuzungumzia maboresho yanayotakiwa yafanyike katika kuimarisha huduma za Afya kwa wagonjwa wanaofika katika Hospitali ya Arusha Jiji. pia Mwenyekiti wa Kikao alihimiza uwajibikaji wa hali ya juu kwa watumishi ikimeo pia suala la lugha nzuri kwa wapokea huduma katika Hospitali ya Arusha Jiji

Tafadhali Andika Maoni Yako

Tafadhali Andika Maoni Yako Hapa kwa Ajira ya Kuboresha Huduma. Karibu sana!!