Huduma ya Lishe
Hospitali ya Jiji Arusha inatoa Huduma mbalimbali za Lishe kupitia kwa Wataalamu wetu wenye uzoefu wa kutosha katika kuhakikisha ubora wa huduma unapatikana zikiwemo;
Huduma za Watoto
- Ushauri juu ya masuala ya Lishe
- Kutoa elimu ya Lishe kwa jamii
- Kutoa ripoti za takwimu za hali ya Lishe katika jamii
Huduma za Watu Wazima
- Ushauri juu ya masuala ya Lishe
- Kutoa elimu ya lishe kwa jamii
- Kutoa ripoti za takwimu za hali ya Lishe katika jamii
Mchanganuo wa Huduma ya Lishe
Huduma mbalimbali za Lishe zinazotolewa katika Hospitali ya jiji Arusha, zinapatikana katika ufanisi wa hali ya juu kulingana na kiwango cha utaalamu kutoka kwa watoa huduma wetu. Pia, huduma hizi zinapatikana kwa kuzingatia makundi tofauti ya wagonjwa wanaokuja kupata huduma kwa makundi ya Watumiaji wa bima ya NHIF, Malipo ya Papo hapo pamoja na aina nyingine za Bima ili kuhakikisha huduma yenye ubora inapatikana. Hospitali ya Jiji Arusha inapenda pia kuwakumbusha watanzania/ wana jamii kuzingatia na kuwa na utaratibu wa kufanya vipimo vya mara kwa mara kwa lengo la kuhakikisha afya zao zinakuwa salama pasipo kusubiri mpaka hali ya afya zao zinakuwa na changamoto / mpaka wanapokuwa wanaumwa.
Miongoni mwa vifaa Tiba zinavyotumika katika kuhakikisha utoaji wa huduma za Lishe katika Hospitali ya Jiji Arusha, ni pamoja na vifaa vya aina mbalimbali kulingana na malengo au madhumuni ya vipimo/ tiba namna au wakati kifaa husika kinahitajika kulingana na tatizo la mpokea huduma kutoka kwa wataalamu wetu wa Afya. Vifaa tiba hivyo ni pamoja na kuzingatia ubora wa hali ya juu
Pia, miongoni mwa dalili za mbalimbali za changamoto za Lishe ambazo Hospitali ya Jiji Arusha inapenda kuwakumbusha watanzania kuwa makini kwa kuchukua tahadhari za haraka pindi wanapokutana nazo ikiwemo kufika katika kituo cha Afya kwa matibabu ya haraka ni pamoja na zifuatazo;
- Mtoto kudumaa kutokana na kukosa lishe bora
- Mama mjamzito kuwa na afya dhaifu
- Upungufu wa damu kwa mtoto na mama mjamzito hasa kipindi cha karibia na kujifungua