Huduma za Ushauri
Hospitali ya Jiji Arusha inatoa huduma mbalimbali za ushauri kwakutumia wataalamu wenye uzoefu wa kutosha katika kuhakikisha ubora wa huduma unapatikana zikiwemo;
Huduma za Watoto
- Ushauri wa Tiba kwa Mazoeiz ya Viungo
- Ushauri wa Masuala ya Lishe bora
- Ushauri wa Daktari
- Ushauri juu ya Masuala ya Uzazi wa Mpango
Huduma za Watu Wazima
- Ushauri wa Tiba kwa Mazoeiz ya Viungo
- Ushauri wa Masuala ya Lishe bora
- Ushauri wa Daktari
- Ushauri juu ya Masuala ya Uzazi wa Mpango
Mchanganuo wa Huduma za Ushauri
Huduma mbalimbali za Ushauri zinazotolewa katika Hospitali ya jiji Arusha, zinapatikana katika ufanisi wa hali ya juu kulingana na kiwango cha utaalamu kutoka kwa watoa huduma wetu. Pia, huduma hizi zinapatikana kwa kuzingatia makundi tofauti ya wagonjwa wanaokuja kupata huduma kwa makundi ya Watumiaji wa bima ya NHIF, Malipo ya Papo hapo pamoja na aina nyingine za Bima ili kuhakikisha huduma yenye ubora inapatikana. Hospitali ya Jiji Arusha inapenda pia kuwakumbusha watanzania/ wana jamii kuzingatia na kuwa na utaratibu wa kufanya vipimo vya mara kwa mara kwa lengo la kuhakikisha afya zao zinakuwa salama pasipo kusubiri mpaka hali ya afya zao zinakuwa na changamoto / mpaka wanapokuwa wanaumwa.
Miongoni mwa vifaa Tiba zinavyotumika katika kuhakikisha utoaji wa huduma za Ushauri katika Hospitali ya Jiji Arusha, ni pamoja na vifaa vya aina mbalimbali kulingana na malengo au madhumuni ya vipimo/ tiba namna au wakati kifaa husika kinahitajika kulingana na tatizo la mpokea huduma kutoka kwa wataalamu wetu wa Afya. Vifaa tiba hivyo ni pamoja na kuzingatia ubora wa hali ya juu