Kambi ya Matibabu ya Madaktari Bingwa wa Mhe. Raisi Samia S. Hassan ndani ya Hospitali ya jiji Arusha
Hii ni kambi ya Matibabu kutoka kwa madakatari bingwa wa Mhe. Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa na lengo la kuimarisha uwezo wa wataalamu wetu katika zoezi zima la utoaji wa huduma bora za afya kwa wagonjwa mbalimbali ndani ya hospitali ya Jiji Arusha
Mganga Mfawidhi, Dr. Salma Kitara akikagua Ujenzi unaoendelea wa Jengo la OPD Complex ndani ya Hospitali ya jiji Arusha
Mganga Mfawidhi Dr. Salma Kitara akifanya Ukaguzi wa Ujenzi unaoendelea wa Jengo la OPD Complex ndani ya Hospitali ya Jiji Arusha ukiwa na lengo la kuimarisha Ufanisi na utoaji wa huduma bora za afya ndani na nje ya halmashauri ya Jiji la Arusha kwa jamii
Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi ndani ya Hospitali ya jiji Arusha
Hii ni sherehe ya Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi iliyofanyika ndani ya Hospitali ya jiji Arusha ikiambatana na maandamano ya Wauguzi mbalimbali ndani ya Jiji la Arusha. Tukio lilienda vizuri na kufurahiwa na watoa huduma wengine mbali na wauguzi
Kliniki ya Mama na Mtoto ndani ya Hospitali ya Jiji Arusha
Ni Kliniki ya Mama na Mtoto (RCH) ikiwa ni miongoni mwa huduma zinazopatikana ndani ya hospitali ya Jiji Arusha ambayo hutolewa kila siku kuanzia saa Mbili kamili asubuhi mpaka saa Tisa na Nusu asubuhi katika kuhakikisha ukuaji na afya bora ya mtoto
Utoaji wa Elimu ya Lishe ndani ya Hospitali ya Jiji Arusha
Ni zoezi la utoaji wa elimu kuhusu lishe lililoendeshwa na Afisa lishe katika ukumbi wa Hospitali. Zoezi likiambatana na mafunzo ya lishe kwa vitengo miongoni mwa washiriki katika kulinda afya za watoto
Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (TANZANIA) ndani ya Hospitali ya Jiji Arusha
Yalikuwa ni Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (TANZANIA) katika viwanja vya Hospitali ya Jiji Arusha ikiambatana na viongozi mbalimbali mgeni rasmi akiwa ni Mkuu wa wilaya ya Arusha Jiji ndugu Mhe. Felician Mtahengerewa shughuli ikiambatana na zoezi la upandaji wa miti pamoja na usafi wa mazingira
Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi ndani ya Hospitali ya jiji Arusha
Hii ni sherehe ya Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi iliyofanyika ndani ya Hospitali ya jiji Arusha ikiambatana na maandamano ya Wauguzi mbalimbali ndani ya Jiji la Arusha. Tukio lilienda vizuri na kufurahiwa na watoa huduma wengine mbali na wauguzi
Ujio wa Timu ya Taasisi na Kudhibiti na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ndani ya Hospitali ya Jiji Arusha
Ulikuwa ni ugeni wa Timu ya Taasisi ya Kudhibiti na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ndani ya viwanja vya Hospitali ya Jiji Arusha ukiambatan na zoezi zima la upandaji wa miti ikiwa ni alama ya kuonesha umoja na mshikamano katika utoaji wa huduma za Afya katika jamii