Matibabu ya Macho
Hospitali ya Jiji Arusha, inatoa huduma mbalimbali za Macho kwa kutumia wataalamu wetu wenye uzoefu wa kutosha katika kuhakikisha Huduma bora inapatikana zikiwemo zifuatazo;
Huduma za Watoto
- Eye Infections diagnosis
- Glass Lens changing
- Eye's Health Consultation
- Eye Infections diagnosis (Eye's Health)
- Test sight ability
- Eye Infections Treatment
- Testing Eye's Pressure (Glaucoma)
Huduma za Watu Wazima
- Eye Infections diagnosis
- Glass Lens changing
- Eye's Health Consultation
- Eye Infections diagnosis (Eye's Health)
- Test sight ability
- Eye Infections Treatment
- Testing Eye's Pressure (Glaucoma)
Mchanganuo wa Matibabu ya Macho
Huduma mbalimbali za Macho zinazotolewa katika Hospitali ya jiji Arusha, zinapatikana katika ufanisi wa hali ya juu kulingana na kiwango cha utaalamu kutoka kwa watoa huduma wetu. Pia, huduma hizi zinapatikana kwa kuzingatia makundi tofauti ya wagonjwa wanaokuja kupata huduma kwa makundi ya Watumiaji wa bima ya NHIF, Malipo ya Papo hapo pamoja na aina nyingine za Bima ili kuhakikisha huduma yenye ubora inapatikana. Hospitali ya Jiji Arusha inapenda pia kuwakumbusha watanzania/ wana jamii kuzingatia na kuwa na utaratibu wa kufanya vipimo vya mara kwa mara kwa lengo la kuhakikisha afya zao zinakuwa salama pasipo kusubiri mpaka hali ya afya zao zinakuwa na changamoto / mpaka wanapokuwa wanaumwa.
Miongoni mwa vifaa Tiba zinavyotumika katika kuhakikisha utoaji wa huduma za Matibabu ya Macho katika Hospitali ya Jiji Arusha, ni pamoja na vifaa vya aina mbalimbali kulingana na malengo au madhumuni ya vipimo/ tiba namna au wakati kifaa husika kinahitajika kulingana na tatizo la mpokea huduma kutoka kwa wataalamu wetu wa Afya. Vifaa tiba hivyo ni pamoja na kuzingatia ubora wa hali ya juu
Pia, miongoni mwa dalili za mbalimbali za matatizo ya Macho ambayo Hospitali ya Jiji Arusha inapenda kuwakumbusha watanzania kuwa makini kwa kuchukua tahadhari za haraka pindi wanapokutana nazo ikiwemo kufika katika kituo cha Afya kwa matibabu ya haraka ni pamoja na zifuatazo;
- Macho kuwasha mara kwa mara na kutoa Machozi
- Uoni hafifu wa Macho
- Kwa watumiaji wa Miwani, Kupungua uwezo wa Miwani katika kuona