Maono

Maono yetu ni kuboresha upatikanaji wa huduma za Afya katika jamii ndani ya Mkoa wa Arusha

Malengo

Pia, Malengo yetu ni kuhakikisha na kuifanyia kazi mikakati yote iliyowekwa katika kuhakikisha ufanisi wa huduma za Afya

Mjadala Mtandao

Shiriki Mjadala Mtandao kwa urahisi kwa kubonyeza kitufe hapo chini


Shiriki Sasa

Salamu za Karibu

Dr. Salma Kitara, Mganga Mfawidhi

Hospitali ya Jiji Arusha ilianzishwa na kuzinduliwa mnamo Tarehe 17 Oktoba, 2021 na Mhe. Raisi Samia S. Hassan, ikiwa ni agizo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuimarisha ufanisi na zoezi zima la utoaji wa huduma za afya ndani ya Halmashauri ya Jiji Arusha


Hospitali ya Jiji Arusha ilianzishwa kwa lengo la kuhakikisha utoaji wa huduma za afya ya uzazi, magonjwa ya kuambukizwa na yasiyo ya kuambukizwa yanadhibitiwa na kuzuiwa katika kiwango kikubwa cha utaalamu wa huduma za afya


Hospitali ya Jiji Arusha inajumuisha Wodi za Mtu Binafsi zaidi ya Nne pamoja na Wodi za Umma zaidi ya Kumi ambao wanakuja kupata huduma katika hospitali


Pia, Hospitali ya Jiji Arusha inatoa huduma kwa wakazi zaidi ya 1000 ndani na nje ya Halmashauri ya Jiji la Arusha katika aina mbalimbali za huduma zikiwemo Wagonjwa wa Nje (OPD), Wagonjwa wa Ndani (IPD), Meno, Macho, Mionzi, Huduma ya Uzazi, Huduma ya Upasuaji, Maabara, Uzazi wa Mpango, Huduma Rafiki kwa Vijana, Huduma ya Mama na Mtoto pamoja na huduma ya Famasi kwa wagonjwa wa malipo ya papo hapo na wa msamaha.

Watumishi
50+
Vifaa Tiba
70+
Samani
150+
Hali ya Usalama

Miongoni mwa Takwimu za huduma zinazotolewa katika Hospitali ya Jiji Arusha zinazotolewa na wataalamu wetu kwa Miaka 4 ya hivi karibuni ni pamoja na zifuatazo;


Kitengo / Mwaka
2021 (Wagonjwa)
2022 (Wagonjwa)
2023 (Wagonjwa)
2024 (Wagonjwa)
ENT Procedure 1483+ 3831+ 3881+ 964+
Gaenacological 9887+ 20828+ 29016+ 7859+
Caesarean 174+ 1148+ 1653+ 410+



Grafu kuonesha muoanisho wa Takwimu za baadhi ya huduma zilizotolewa katika Hospitali ya Jiji kwa Miaka 4 ni kama ifuatavyo;


Matangazo

- Mpango wa Kuboresha Huduma za Afya

- Ujio wa Mhe. Ally Hapi

Matukio Yajayo

- Siku ya Pasaka April 20, 2025

- Siku ya Eid ul Fitr Mar 31, 2025

Huduma Zetu

Miongoni mwa huduma zinazotolewa katika Hospitali ya Jiji Arusha ni pamoja na zifuatazo.

Huduma ya Mionzi

Hospitali ya Jiji Arusha inatoa huduma bora ya Mionzi kwa kuzingatiwa viwango vya hali ya juu vya utaalamu


Peruzi Zaidi

Huduma ya Upasuaji

Wagonjwa wanapata pia huduma ya Upasuaji ya kiwango cha ubora wa hali ya juu. Hivyo Wataalamu wetu wanahakikisha katika utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa wenye matatizo mbalimbali


Peruzi Zaidi

Huduma ya Kupima

Pia, Huduma ya Kupima inapatikana ndani ya hospitali ya jiji Arusha kutoka kwa wataalamu wetu wabobezi. Hivyo, ufanisi wa huduma kwa wagonjwa wetu unapatikana


Peruzi Zaidi

Huduma ya Maabara

Huduma ya Maabara ya kiwango cha hali ya juu inatolewa kutoka kwa wataalamu wetu wazoefu katika kuhakikisha huduma bora inatolewa kwa wagonjwa wenue matatizo mbalimbali


Peruzi Zaidi

Huduma ya Famasi

Wataalamu wetu wa Famasi wapo tayari kukuhudumia kwa kuzingatia huduma ya kiwango cha hali ya juu. Hivyo, wagonjwa wenye matatizo mbalimbali wanapatiwa huduma ya Matibabu inayostahili


Peruzi Zaidi

Huduma ya Macho

Pia, Huduma ya Macho inapatikana ndani ya Hospitali ya Jiji Arusha kwa kuzingatiwa kiwango cha hali ya juu kwa kutumia vifaa vyenye kiwango cha hali ya juu.


Peruzi Zaidi

Appointment ya Daktari

Tafadhali jaza taarifa zinazohitajika kufanya Appointment na Daktari

Wasiliana Nasi

(+255) 682 136 704

Tuma Ujumbe

ach@arushacc.go.tz

Eneo Tulipo

Njiro, Contenna. S.L.P 3013 Arusha. TANZANIA

MATUKIO

Ndani ya Hospitali ya Jiji Arusha, kuna matukio mbalimbali yanayotokea yakihusisha na zoezi zima la utaoji wa huduma bora ya Afya kutoka kwa wataalamu wetu wabobezi kama ifuatavyo

Maendeleo ya Ujenzi wa Jengo la OPD Complex ndani ya Hospitali ya Jiji Arusha

Ni moja ya sehemu inayoonesha maendeleo ya Ujenzi wa Jengo la OPD Complex ndani ya Hospitali ya jiji Arusha ikiwa ni moja ya maagizo ya serikali katika kuimarisha huduma za afya ndani ya jiji la Arusha

Peruzi Zaidi

Ugeni wa Benki ya NCBA ndani ya Hospitali ya Jiji Arusha kama mdau wa Huduma za Afya

Ulikuwa ni muda mzuri kuikaribisha timu ya Benki ya Benki ya NCBA ndani ya Hospitali ya Jiji Arusha, zoezi likiambatana na upandaji wa miti kama ishara ya ushirikiano katika huduma za afya.

Peruzi Zaidi

Ujio wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha (Mhe. Paul Makonda) ziara ya kutembelea ujenzi wa Jengo la OPD Complex

Ni ziara ya kutembelea ujenzi wa Jengo la OPD Complex ikiwa ni moja ya agizo la serikali katika kuboresha sekta ya Afya kupitia mikikati ya miundombinu na vitendea kazi vya kutolea huduma kwa jamii

Peruzi Zaidi

Kambi ya Matibabu ya Madaktari Bingwa wa Mhe. Raisi Samia S. Hassan ndani ya Hospitali ya jiji Arusha

Hii ni kambi ya Matibabu kutoka kwa madakatari bingwa wa Mhe. Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa na lengo la kuimarisha uwezo wa wataalamu wetu katika zoezi zima la utoaji wa huduma bora za afya kwa wagonjwa mbalimbali ndani ya hospitali ya Jiji Arusha

Peruzi Zaidi

Semina ya Mafunzo ndani ya Tume ya Taifa ya Mionzi Tanzania(TAEC) Njiro, Arusha

Hii ni Semina na Mafunzo iliyotolewa katika ofisi za Tume ya Taifa ya Mionzi (TAEC) Njiro, Arusha ikijumuisha wataalamu wetu wa Afya ikiwa na lengo la kutoa elimu ya Ushauri kuhusu masuala ya Afya kutoka kwa wataalamu wetu kuhusu matatizo mbalimbali ya afya

Peruzi Zaidi

Mganga Mfawidhi, Dr. Salma Kitara akikagua Ujenzi unaoendelea wa Jengo la OPD Complex ndani ya Hospitali ya jiji Arusha

Mganga Mfawidhi Dr. Salma Kitara akifanya Ukaguzi wa Ujenzi unaoendelea wa Jengo la OPD Complex ndani ya Hospitali ya Jiji Arusha ukiwa na lengo la kuimarisha Ufanisi na utoaji wa huduma bora za afya ndani na nje ya halmashauri ya Jiji la Arusha kwa jamii

Peruzi Zaidi

Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi ndani ya Hospitali ya jiji Arusha

Hii ni sherehe ya Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi iliyofanyika ndani ya Hospitali ya jiji Arusha ikiambatana na maandamano ya Wauguzi mbalimbali ndani ya Jiji la Arusha. Tukio lilienda vizuri na kufurahiwa na watoa huduma wengine mbali na wauguzi

Peruzi Zaidi

Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (TANZANIA) ndani ya Hospitali ya Jiji Arusha

Yalikuwa ni Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (TANZANIA) katika viwanja vya Hospitali ya Jiji Arusha ikiambatana na viongozi mbalimbali mgeni rasmi akiwa ni Mkuu wa wilaya ya Arusha Jiji ndugu Mhe. Felician Mtahengerewa shughuli ikiambatana na zoezi la upandaji wa miti pamoja na usafi wa mazingira

Peruzi Zaidi

Ujio wa Timu ya Taasisi na Kudhibiti na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ndani ya Hospitali ya Jiji Arusha

Ulikuwa ni ugeni wa Timu ya Taasisi ya Kudhibiti na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ndani ya viwanja vya Hospitali ya Jiji Arusha ukiambatan na zoezi zima la upandaji wa miti ikiwa ni alama ya kuonesha umoja na mshikamano katika utoaji wa huduma za Afya katika jamii

Peruzi Zaidi

Utoaji wa Elimu ya Lishe ndani ya Hospitali ya Jiji Arusha

Ni zoezi la utoaji wa elimu kuhusu lishe lililoendeshwa na Afisa lishe katika ukumbi wa Hospitali. Zoezi likiambatana na mafunzo ya lishe kwa vitengo miongoni mwa washiriki katika kulinda afya za watoto

Peruzi Zaidi

Kikao cha Mpango Bajeti ya Vitengo Hospitali ya Jiji Arusha

Hiki ni kikao kilichokuwa kinazungumzia bajeti na mipango mbalimbali ya vitengo vinavyotoa huduma katika hospitali ya Jiji Arusha ikiwemo kufanya tathmini na kuchambua masuala mbalimbali yanayohusiana na vitengo katika kuboresha utoaji wa huduma za afya

Peruzi Zaidi

Kliniki ya Mama na Mtoto ndani ya Hospitali ya Jiji Arusha

Ni Kliniki ya Mama na Mtoto (RCH) ikiwa ni miongoni mwa huduma zinazopatikana ndani ya hospitali ya Jiji Arusha ambayo hutolewa kila siku kuanzia saa Mbili kamili asubuhi mpaka saa Tisa na Nusu asubuhi katika kuhakikisha ukuaji na afya bora ya mtoto

Peruzi Zaidi

Kalenda

Miongoni mwa Taarifa, Kalenda na Ratiba za Vikao mbalimbali ndani ya Hospitali ya jiji Arusha ni pamoja na kama ifuatavyo

52+

Vitanda

7859+

Huduma za Upimaji

964+

Huduma za Upasuaji

964+

Kliniki

Wadau Wetu

Wodi za Wagonjwa

Tafadhali weka Booking ya Wodi za Wagonjwa kwa urahisi kwa kubofya Kitufe hapo chini

Wodi ya Umma

Admin

Tuna Wodi za Umma zenye ubora wa kiwango cha hali ya juu kwa wagonjw wanaofika kwa ajili ya kupata huduma za matibabu

Fanya Booking

Wodi za Mtu Binafsi

Admin

Weka Booking ya Wodi za Mtu Binafsi zenye ubora wa hali ya juu kwa ajili ya wagonjwa wanaofika kupata huduma kwa kubofya kitufe hapo chini

Fanya Booking

Wodi za Dharula

Admin

Pia, tuna Wodi za Dharula kwa ajili ya wagonjwa wanaofika kupata huduma ndani ya Hospitali ya Jiji Arusha

Fanya Booking